·
Baada
ya kufariki Mangwea, Langa naye “achomoka.”
Na. Deo Kaji Makomba.
Tasinia ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania,
imepatwa pigo jingine baada ya kuondokewa na mwanamuziki mwingine ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzikwa
kwa mwanamuziki Albert Mangwea, aliyefariki dunia huko nchini Afrika ya kusini
na kuzikwa mkoani Morogoro.
Mwanamuziki aliyefariki dunia wakati huu ni Langa Kileo, almaarufu Langa, mzee wa
matawi ya juu.
Taarifa zilizopatika hapo jana majira ya jioni kutoka
katika vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mitandao ya kijamii, na kukifikia
chumba chetu cha habari cha mtandao huu ,zimeeleza kufariki dunia kwa
mwanamuziki huyo ambaye pia aliwahi kufanya vyema katika tasinia ya muziki wa
kizazi kipya wakati ule akichomoka akiwa na kundi zima la wakilisha.
Langa akiwa na kundi hilo aliweza kutikisa na wimbo
wao wa Kiswangilishi, huku akiendelea kutamba na rekodi nyingine ikiwemo ile
iliyojulikana kwa jina la matawi ya juu.
Kabla ya kifo cha mwanamuziki huyo kutokea, alikuwa
akitamba na rekodi mpya aliyoitoa takribani wiki mbili zilizopita, rekodi
iliyojulikana kwa jina la rafiki wa kweli.
Kifo cha Langa, kimetokea katika hospital ya rufaa ya
Muhimbili, ambapo mwili wa marehemu, umehifadhiwa huko na taratibu za mazishi
zikiendelea kufanyika.
No comments:
Post a Comment