Tuesday 23 July 2013

HARAKATI ZA KUWANIA UBINGWA LIGI KUU YA SOKA YA VODACOM TANZANIA BARA.



·        TFF yatoa ratiba, kivumbi kuanza kutimka agost 24
·        Timu zote 14 kufungua pazia la michuano hiyo. 

                  Na.  Deo Kaji Makomba.

 Hekaheka za kuwania ubingwa wa ligi kuu yasoka ya Vodacom Tanzania bara, zinatarajia kuanza hapo mwezi agost 24 mwaka huu, huku kukishuhudiwa jumla ya timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo zikiingia katika viwanja tofauti kukata utepe katika ligi kuu hiyo ya msimu huu.

Lakini kabla ya kuanza kwa kindumbwendumbwe hicho cha ligi kuu ya soka Tanzania bara, kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).

Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).


No comments:

Post a Comment