Thursday 8 August 2013

UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JULIUS NYERERE JIJINI DAR NA MADAI YA KUTUMIKA KUPITISHIA "UNGA"



Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere nchini Tanzania, katika kashifa ya u madawa ya kulevya.

·     Yaelezwa uwanja huo watumika kama kichaka cha kupitishia dawa za kulevya



·     Waziri Mwakyembe ataka mamlaka husika kuchukua hatua za haraka.

.
                   Na. Mwandishi wetu

Nchini Tanzania kutajwa kwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuwa ni mmojawapo wa njia kuu za kusafirisha madawa ya kulevya, kumeibua mjadala mzito nchini humo wa namna ya kudhibiti biashara hiyo haramu.

katika siku za hivi karibuni baadhi ya raia wa Tanzania wamekuwa wakishikiliwa katika mataifa mbailimbali ya nje ikiwemo China, Brazil, Afrika kusini na Thailand kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya suala lililozua hoja ya udhaifu katika udhibiti kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam ambako madawa hayo hupitishwa.

Waziri wa uchukuzi wa Tanzania Dakta Harrison Mwakyembe, katika moja ya shughuli zake za kikazi kwenye  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, aliibua sakata hilo la uwanja huo wa ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere kuwa kichaka cha kupitisha dawa za kulevya na kutaka hatua za haraka kuchukuliwa na mamlaka husika kwani kashfa hiyo inaharibu taswira nzuri ya taifa, hasa ukizingatia kuwa uwanja huo unabeba jina la baba wa taifa la Tanzania.

Waziri Mwakyembe ambaye alikuwa akizindua rasmi kamati mpya ya taifa ya usalama wa usafiri wa anga, ameitaka kamati hiyo kuacha kufanyakazi kwa kuogopa wakubwa na kusisitiza kwamba hadhi ya Tanzania imeshuka mno mbele ya macho ya kimataifa kutokana na kashfa hiyo ya madawa ya kulevya hivyo hawana budi kutafuta majawabu ya kwa nini viwanja vya ndege vya Tanzania vimekuwa uchochoro wa kusafirisha madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment