Sakata la Luis Suarez kutaka kuikacha Liverpool kuelekea Asernal;
· Bosi wa Liverpool Brendan Rodgers, amtaka Suarez kujikosoa
· Asema Suarez ameonesha dharau kubwa licha ya kupewa kila kitu na klabu hiyo.
Na.
deo
kaji makomba.
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Liverpool,
Luis Suarez, ametakiwa na bosi wa klabu hiyo, Brendan Rodgers kujikosoa na
kujifunza yeye mwenyewe, na kuongeza kuwa Suarez ameonesha dharau kubwa kwa
majogoo hao wa Anfeld.
Rodgers pia amepinga madai ya
mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay ya kwamba aliahidiwa ataondoka ndani ya klabu
hiyo katika msimu huu wa kiangazi endapo kama Liverpool haitashinda katika ligi
ya mabingwa barani ulaya.
Suarez mwenye umri wa miaka 26, yuko
katika mpango wa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho wiki hii kama mchakato
wake wa kuelekea kwa washika bunduki wa London, Asernal the Gunners, utazuiliwa
na uongozi wa Liverpool.
“Hakukuwa na ahadi yoyote
iliyotolewa na hakuna ahadi iliyovunjwa.” Alisisitiza Rodgers.
“Klabu na mwakilishi wa mchezaji
huyo, wamekuwa na mazungumzo na alijua sahihi wapi alikuwa.
“Amekuwa dharau ya hali ya juu kwa
klabu, klabu ambayo ilimpatia mchezaji huyo kila kitu.” Alisema bosi huyo wa Liverpool.
No comments:
Post a Comment