Thursday 8 August 2013

SEKESEKE LA USAJILI HUKO BARANI ULAYA, SAFARI HII



Barcelona watupa karata kutaka kumchukua mlinzi wa Chelsea, David Luiz

·        Chelsea yatolea nje ofa hiyo



·        Yasema ingali inamuhitaji mchezaji huyo

                  
                    Na. deo kaji makomba

Wakati sekeseke la usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu mbalimbali huko barani ulaya likiendelea huku vilabu mbalimbli barani humo vikichuana huku na kule kuweza kuona vinasajili vikosi imara katika msimu mpya wa ligi kuu mbalimbali barani humo, klabu ya kandanda  Chelsea ya England,imepokea ofa kutoka klabu cha kandanda cha Barcelona cha nchini uispania, kikimtaka mlinzi wa kimataifa wa Brazil, David Luiz aichezee klabu hiyo yenye masikani yake Jijini Barcelona.

Mlinzi huyo wa kimataifa wa Brazil, mwenye umri wa miaka 26, ambaye alijiunga na Chelsea akitokea Benfica ya Ureno kwa dau la paun milioni 21 mnamo mwezi januari mwaka 2011, amekuwa akiangaliwa husuda na vigogo hivyo vya soka nchini Uispania.

Lakini wakati Barcelona wakionesha nia ya kumtaka David Luiz kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya soka ya nchini Uispania, kwa upande wao Chelsea mara zote wamesisitiza kuwa, Luiz ambaye amekwishaichezea klabu hiyo zaidi ya mechi 100, katu hawatamuuza.

Ofa hiyo kutoka Barcelona, inatarajiwa kuwa ya pesa tasilimu na kwamba mkataba huo hautahusisha mabadilishano ya mchezaji yeyote kutoka Barcelona.

Barcelona hivi sasa iko chini ya uongozi wa kocha kutoka nchini Argentine, Gerardo Martino, amekwishakamilisha kusainisha walinzi wa kati.

David Luiz akitokea Benfica ya Ureno, alinunuliwa kwa dau la pauni milioni 21 hapo januari 31 mwaka 2011 na ikicheza mechi 109 akiwa na klabu hiyo ya Ureno katika mashindano yote na akifunga magoli 12

Mchezaji Veteran wa soka Carles Puyol aliyekuwa na tatizo la goti katika msimu uliopita na umri wake wa miaka 35 alifanyiwa upasuaji mnamo mwezi machi wakati walinzi wenzake Gerard Pique, Adriano correia na Javier Mascherano walikuwa na majeruhi au kuwa na adhabu kwa nyakati tofauti katika mashindano mbalimbali.

Naye mlinzi wa kati wa Paris St-Germain ya Ufaransa, Thiago Silva, alikuwa akihusishwa na mchakato wa kutaka kujiunga na Barcelona yenye masikani yake Nou Camp, lakini mlinzi huyo wa kati wa kimataifa wa Brazil akasaini mkataba na mabingwa wa Ufaransa mwezi uliopita.

Luiz alicheza dakika 30 wakati Chelsea ikicheza mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Inter Milan alhamisi iliyopita, lakini aliondolewa kutoka katika kikosi cha Jose Mourinho, katika mechi dhidi ya timu yake ya zamani aliyokuwa akiifundisha ya Real Madrid, huko Miami.

No comments:

Post a Comment