Waingereza washambuliwa Zanzibar
Ni mara ya kwanza kwa shambulizi
kama hili kutokea Zanzibar
Polisi katika kisiwa cha Zanzibar
wamesema wanawake wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao
baada ya kuvamiwa mwendo wa usiku.
Naibu kamishna wa polisi amesema
kuwa wanaume wawili waliwatendea wanawake hao Katie Gee na Kirstie Trup, wote
wenye umri wa miaka 18 kutoka London,kitendo hicho walipokuwa wakitembea katika
barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.
Wanawake hao ni walimu wa kujitolea
wakifanya kazi kisiwani humo
Amesema kuwa polisi tayari
wameanzisha msako dhidi ya wanaume hao.
Katika taarifa yake shirika la
usafiri la i-to-i nchini Uingereza lilisema kuwa wanawake hao wameondoka
hospitalini.
Kwa upande wake wizara ya mambo ya
ndani Uingereza ililezea wasiwasi kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wake na
kuwa tayari imetoa msaada kwao kupitia kwa ubalozi wake.
Wanawake hao, wanasemekana kufanyia
kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi hilo haijulikani.
Polisi wanasema kuwa wanawake hao
wenye umri wa miaka 18 walikuwa wakitembea katika mji wa Mawe kisiwani Zanzibar
ambao ni kivutio kikuu cha utalii kisiwani humo, wakati wanaume wawili
waliokuwa wamepanda piki piki walipowamwagia Acid kwenye mikono , vifua na
nyuso zao.
Wanawake hao walipelekwa kwa ndege
hadi Dar es Salaam ambako walipokea matibabu . Afisa wa wizara ya afya amesema
kuwa majeraha yao si ya kutishia maisha .
Polisi wa Zanzibar wamesema ni mara
ya kwanza kwa raia wa kigeni kushambuliwa kwa namna hiyo na kwamba wanawasaka
wahusika.
Zanzibar ni kisiwa kinachokaliwa na
idadi kubwa ya waislam na shambulio hilo linakuja katika kipindi cha mwisho wa
mwezi mtukufu wa Ramadhan , wakati watu wakisherehekea sherehe za Eid
No comments:
Post a Comment