Thursday 8 August 2013

BAADA YA KULIPUKA KWA MOTO KWENYE UWANJA NDEGE HUKO KENYA



Shughuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata zarejea katika hali yake ya kawaida.


Habari hizi na mashirika ya habari

Shughuli katika uwanja wa kimataifa wa ndege JKIA nchini Kenya, zinatarajiwa kurejea katika hali ya kawaida kuanzia usiku wa manane.

Waziri wa usafiri, Michael Kamau, amesema kuwa sehemu iliyotengewa marasia kuingilia na kutoka kwenye uwanja hyuio itatumiwa na wageni kutoka nchi za kigeni watakaowasili katika uwanja huo.

Safari kadhaa za ndege za kimataifa zilirejea leo huku ndege za shirika la ndege la Kenya zikitua na kuruka katika hali inayoweza kusemekana kuwa ya kawaida.

Ndege za kimataifa zimeanza kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa jijini Nairobi JKIA, siku moja tu baada ya kitengo cha kuwasili wageni kuchomwa na moto mkubwa na kulazisha uwanja huo kufungwa kwa masaa kadhaa.

Ndege ya kwanza ya kimataifa kuwasili katika uwanja huo ni ile iliotoka Uingereza na baadaye nyengine kutoka Tanzania na Bangkok zikawasili.

Wachunguzi hata hivyo wanatathmini chanzo chake.

Wakati huo huo Rais wa Marekani, Barack Obama amesema ataisaidia serikali ya Kenya katika kukarabati uwanja huo wa ndege baada ya moto mkubwa kuuteketeza hapo jana.

Katika ujumbe wake wa simu, Obama alisisitiza kuwa Marekani iko tayari kuisadia Kenya katika hali ile yoyote kutokana na ushikiano wake na Kenya.

Obama pia aliwapa pole familia zilizowapoteza wapendwa wao katika mashambulizi ya bomu ya Agosti 1998 mjini Nairobi.

Manmo Jumatano, moto mkubwa uliotokea majira ya asubuhi, uliharibu kitengo cha kuwasilia wageni wa kimataifa.

Vikundi vya wachunguzi viliwasili katika uwanja huo kufanya uchunguzi wao kubaini kilichosababisha moto huo.

Abiria walikwama kutokana na mkasa huo ingawa waliweza kuondolewa nje ya uwanja kwa ajili ya usalama wao huku baadhi wakiangalia mizigo yao ikiteketea wasijue la kufanya. .

Rais Uhuru Kenyatta aliwasili katika uwanja huo na kujionea uharibifu uliotokea na kiisha kutoa taarifa yake kupitia kwa msemaji wake Esipisu aliyesema kuwa chanzo cha moto huo kinachunguzwa.

Wapelelezi wanaendelea na uchunguzi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata mjini Nairobi, kufuatia moto mkubwa uloanza Jumatano alfajiri na kuteketeza jengo la mapokezi ya abiria wa kimataifa.


No comments:

Post a Comment