Thursday 8 August 2013

KUELEKEA KINDUMBWENDUMBWE CHA LIGI KUU YA SOKA YA ENGLAND.


 “Wayne Rooney hayuko kifedha zaidi” Owen.



 

           Na. deo kaji makomba

Maamuzi ya mhambuliaji wa timu ya soka ya Manchester United, Wayne Rooney ya eidha  kubaki katika klabu hiyo yenye masikani yake Old Traford hayatachochewa na fedha, hiyo ni kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani Michael Owen.

Rooney tayari amehusishwa mchakato wa kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo ya mashetani wekundu,licha ya klabu hiyo iliyo chini ya kocha mpya hivi sasa David moyes, ikisisitiza kuwa Roney hauzwi.
Owen aliiambia BBC Sport, “Wayne Rooney hayuko kwa ajili ya kutaka kulipwa malipo makubwa. Yuko kwa minajili ya kucheza soka.

“Anapenda sana mpira, na si fedha. Anataka kuwa akicheza soka muda wote katika mashindano makubwa.”

Owen mwenye umri wa miaka 33, alicheza na Rooney katika timu ya taifa ya England pamoja na klabu ya Manchester united kabla ya kutundika daruga kuachana na soka mwishoni mwa msimu uliopita.

Anaamini kuwa Roney mwenye umri wa miaka 27, anapenda kubaki Old Trafford lakini anahofia hana muda mrefu kubakia katika chaguo la kikosi cha kwanza ndani ya Manchester United.

Rooney hakuhusishwa ndani ya kikosi katika ligi ya mabingwa kilichofungwa na Real Madrid hapo mwezi machi na meneja mpya wa Manchester United, David Moyes, akieleza kuwa Rooney hatokuwa katika chaguo lake katika kikosi cha kwanza, mapema katika wakati huu wa kiangazi huku Robin Van Persie akionekana ni mshambuliaji namba moja katika kikosi cha kwanza cha mashetani hao wekundu.

United wamekwishakataa ofa mbili kutoka Chelsea ikiwemo ile yenye thamani ya pauni milioni 25 na nyongeza nyingine

Owen amesema: “Kiuhakika Wayne atapenda kubaki Machester United, akicheza kila mchezo. Swali kubwa hapa Manchester United itampa uhakika wa kuwemo katika kikosi cha kwanza?

“Nashindwa kuelewa kwanini watu wanazungumza  pesa wakati wote. Wayne Rooney yuko sawa katika suala la pesa na hakuna mtu anayetakiwa kuwa na wasiwasi kuhusiana na kipato kuongezeka.
“Baada ya kumjua kwa muda mrefu Rooney  na naweza kukuhakikishia hayuko kifedha

No comments:

Post a Comment