Sunday 27 October 2013

BILALI WA TOTO ABWAGA MANYANGA



Kikosi cha timu ya Toto Afrikan kabla timu hiyo haijashuka daraja kutoka ligi kuu
Kocha wa timu ya Toto aachia ngazi.

  • ·      Ni Athumani Bilali.

  • ·      Sababu ni ukata wa fedha unayoikabili timu hiyo.


            Na. Mashaka Baltazar

WAKATI Toto African Jijini Mwanza ikiwalaza vinara wa ligi Daraja la Kwanza kundi C,Stendi United ya Shinyanga,kocha wa timu hiyo, Athuman Bilal,amejiondoa kukinoa kikosi hicho.

Akizungumza na gazeti jana muda mfupi baada ya mchezo huo ambao Toto ilishinda kwa bao 1-0,Bilal alisema sababu kubwa ya kuachia ngazi kuifundisha timu hiyo,inatokana na ukata,hiyo bora aachie ngazi kulinda heshima yake.

Alisema haoni haja ya kuendelea kuwa na kikosi hicho,wakati timu inakabiliwa na ukata na wachezaji wanalishe duni,hali inayochangia washindwe kufanya mazoezi ya pamoja.

“Ushindi huu umepatikana kwa juhudi za wachezaji,wamejituma lakini hali waliyo nayon ni njaa tupu.Huwezi kucheza mpira ukiwa na njaa, hali ni ngumu na siwezi kuendelea kuwa na timu hii.”

“Maandalizi ni mabovu,wachezaji hawafanyi mazoezi kwa pamoja na hii ni mechi yangu ya mwisho.Nittaangalia maisha yangu kuona wapi naelekea.Timu hii ni ngumu na inahatarisha maisha ya waachezaji.”alisma Bilal

Kocha huyo ambaye amedumu na Toto kwa misiimu kadhaa sasa. ameutaka uongozi wa klabu hiyo uliopo ujipange kama unahitaji kupata mafanikio vinginevyo ni ndoto za mchana kufanya vizuri.

Msemaji wa Toto Omar Mbalamwezi alipotafutwa n gazeti hili ,kujua hatma ya kumpata kocha mbadala wa Bilal, hakupatikana

Hadi sasa Toto ina pointi nane baada ya  kushuka dimbani mara 6 katka mzunguko waa kwanza,hivyo inahitaji nguvu ya ziada katika duru la pili kuona kama inashuka ama inabaki daraja la kwanza.

No comments:

Post a Comment