Sunday 27 October 2013

WANANCHI WATAKIWA KUJITOLEA DAMU





 Katibu wa Wasanii Mkoa wa Mwanza, Hussein Kim,akipima mapigo ya moyo kabla ya kutolewa damu .Wasanii hao walijitolea kuchangia damu lit zaidi ya 200.


·        
Jamii yatakiwa kujenga utamaduni wa kujitolea damu.


  • Ili kuondokana na upungufu wa damu katika hospital kanda ya ziwa

  • Wasanii wa kanda ya ziwa wajitolea damu.

 

                           Na. Mwandishi wetu.


WASANII mbalimbali  wa Kikundi cha MET Club cha Jiji la Mwanza, wameitaka Jamii kujenga tabia na utamaduni wa kuchangia damu kwa hiari, ili kuokoa maisha ya watu.
Mwuuza magazeti wa Jiiji la Mwanza (Kulia ) akijitolea kucangia damu katika zoezi lilofanyika jana likijumuisha wWaasanii wa Jiji la Mwanza, MET Club.
 
Kwamba uchangiaji damu kwa hiari, utasaidia kukabiliana na upungufu wa changamoto ya damu katika hospitali za mikoa ya Kanda ya Ziwa,ambazo hupata huduma hiyo, kutoka Kituo cha Taifa cha Damu Salama, Bugando.
Mtumishi wa Kituo cha Damu Salama Mwanza akitolewa damu katika zoezi la changia damu okoa masiha lililoendeshwa na wasaniii wa Mwanza, MET Club

Mwenyekiti wa MET Club, Ramadhan Said, akizungumza katika tamasha la kuchangia damu lenye kauli mbiu ya Okoa Maisha ambalo lililowahusisha wasanii hao, alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini changamoto ya ukosefu wa damu ni kubwa katika hospitali zetu.

Alisema Wasanii kama kioo cha Jamii,na kwa  kitendo chao cha kuchangia damu,kimeweka alama kwenye vichwa vya watu watambue tatizo na kujenga moyo wa kujitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu .

“Wasanii tumetengezwa ili kufanya kazi za jamii.Tumeguswa baada ya kuona tatizo la damu ni kubwa,ambapo baadhi ya hospitali zinawauzia wagonjwa damu,wakati inatolewa bure.Tukaona bora tuchangie sisi kwanza ili kuhamasisha jamii kufanya hivyo,”alisema Said

Awali Katibu wa Wasanii Mkoa wa Mwanza, Hussein Kim,alisema mbali na wao kuguswa,lakini pia ni wajibu wa kila Mtanzania kuona umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wengine bila kujali dini,rangi,kabila wala itikadi.

“Tumeanza kuwa mfano na  jamii iwe tayari kutuunga mkono. Kama tunashindwa kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama na watoto,ambao wengi wao hupoteza maisha kwa kukosa damu, hatupaswi kulaumu.Niseme zoezi hili litakuwa endelevu,”alisema Kim.

Alisema akina mama na watoto ndiyo wahanga wakubwa, ambao vifo vyao vingi vinasababishwa na ukosefu wa damu katika hospitali mbalimbali za Jijini hapa na kote nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Mwanza (TDFAA) Abdallah Ramadhan,alisema katika tamasha hilo,waliweka lengo la kuchangia lita 200 za damu ambalo wamefanikiwa kulivuka.

No comments:

Post a Comment