Sunday 27 October 2013

UCHAGUZI MKUU TFF LEO

 Lufano aanika ajenda zake TFF
                                     
                                  Na. Mashaka Baltazar.

WAKATI Uchaguzi wa mkuu wa Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), unafanyika leo,Vedastus Lufano,anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji, amewataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa shirikisho hilo, wamchague kama wanahitaji mabadiliko na maendeleo ya mpira.

Alisema wakimchagua kushika wadhifa huo,atashirikiana na viongozi wenzake wa TFF,  kutaleta mabadiliko chanya na yenye tija ili kuutendea haki mpira wa miguu na wadau wa mchezo huo.

Akizungumza na Kisima cha habari muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea Jijini Dar es salaam jana, Lufano anayewania nafasi hiyo kupitia mikoa ya Mara na Mwanza,alisema akichaguliwa kwenye taasisi hiyo ya soka,atashawishi yafanyike maboresho ya chagamoto zinazodumaza maendeleo ya mpira wa miguu.

“Soka letu linahitaji mabadiliko ya kweli.Lazima soka la vijana lipewe kipaumbele kuelekea kwenye mafanikio.Katika hali ya kawaida, huwezi kupata maendeleo ya mpira bila uwekezaji soka la watoto wadogo na vijana.Hiyo ni agenda yangu ya kwanza pamoja na timu yote ya TFF,” alisema Lufano

Alisema Tanzania inashindwa kupiga hatua kwenye soka sababu ya viongozi waliopewaa dhamana wakati hawana dhamira ya kuendeleza mchezo huo.Yeye kama familia ya soka, atahakikisha kunakuwa na mapinduzi kwenye mpira wa Tanzania.

“Tuna vipaji vingi vya soka kila kona ya nchi yetu,lakini inavyoonekana mpira umebaki wa eneo moja tu.Kwa staili hiyo hatuwezi kupata maendeleo na ndiyo maana nasema, lazima mapinduzi yawepo katika soka yetu na  ikiwezekana tutengeneze mfumo mpya mbadala wa uliopo sasa,”alisema  Lufano

Alisema kwa kushirikiana na timu nzima ya TFF itakayochaguliwa akiwemo yeye, hilo linawezekana na kusisitiza uwekezaji wa soka ya watoto wadogo na vijana ili kujenga msingi na mfumo bora, utakaosaidia kuwa na timu imara ya Taifa.

Mbali na kulilia soka ya watoto na vijana, atajielekeza kwenye soka ya wanawake pamoja na kutetea maslahi ya waamuzi, ambao ni wadau wa mpira wa miguu ili kuwaepusha na vishawishi wafanye kazi yao kwa uadilifu.

Lufano ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF Mkoa wa Mwanza, katika kinyang’anyiro hicho anapambana na Jumbe Odesa Magati na Samwel Nyalla (Mwanza) na Mugisha Galibona kutoka Mara.

WAKATI hayo yakichomoza, mmoja wa wagombea wa nafasi ya juu kwenye uchaguzu huo, anadaiwa kuwahonga wajumbe wa mkutano huo.
Mgombea huyo anadaiwa kutoa kitita cha fedha kwa wajumbe wa mkutano huo, ambapo aliwatumia baadhi fedha za tiketi za ndege,kwenda kushuhudia mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga.
Mmoja wa watu wa kambi ya mgombea huyo, Alfred Lwiza,alikakaririwa na mwandishi wa habari hizi, akisema mgombea mmoja amewatumia tiketi za ndege  wajumbe.
“Hivi tunavyozungumza mmoja wa wagombea ametutumia tiketi za ndege wajumbe wote wa Mkutano Mkuu, tukashuhudie mechi ya Simba na Yanga,”alisema Lwiza 
Ni kauli hiyo iliyozua mahojiano kati ya Lwiza  na mwandishi wa gazeti hili kwenye uwanja wa CCM Kirumba, akihoji tiketi na gharama zingine kwa wajumbe hao ni rushwa ama ni fadhila.
Kwamba ikitokea amechaguliwa kushika wadhifa huo wa juu wa TFF,atatumia muda wake kurejesha fedha zake badala ya kuutendea haki mpira.
Lwiza katika majibu yake alisema, hizo ndizo faida (privarage) za mpira, kwamba hata baadhi ya waandishi wa habari wanaothaminiwa na mgombea huyo wamelipwa fedha wamwandike vizuri.
“Wewe utaendelea kuongea hapa na kuandika,huo ndio mpira unachezwa ndani na nje ya uwanja.Kwa taarifa yako hata waandishi wa habari wenzako wanaothaminiwa wamepewa fedha,”alisema Lwiza
Mkufunzi huyo wa Waamuzi, alipobanwa kuwa hiyo ni rushwa ya kuwalainisha wajumbe wa mkutano huo ili wamchague kiongozi huyo hata kama uwezo hana, alisema “wewe wasema sijui rushwa ama takrima,ukweli ndiyo huo.”
Aidha wadau waliokuwapo uwanjani hapo walisema,ni vigumu mpira wa Tanzania kuendelea kwa sababu ya wajumbe aina ya Lwiza, ambao wanatanguliza rushwa mbele katika kuchagua viongozi.
“Kila mara tunalalamika mpira wetu hauendelei, sababu ya wajumbe wa kama  Lwiza.Wanatanguliza maslahi yao kwa kupokea rushwa, kisha wanatuchagulia viongozi wabovu,”alisema mdau mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Juma
Hata hivyo baadhi walisema wa kulaumiwa ni Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na  Rushwa nchini (TAKUKURU),sababu rushwa kwenye uchaguzi huo iko nje nje .
Walisema wanaweza ama wangeweza kudhibiti rushwa hivyo kwa kufuatilia mitandao ya siu za wajumbe na wagombea.Lakini kwa hali ilivyo ni wazi tutapata viongozi wasio stahili ambao hawatautendea haki mpira wa miguu sababu ya rushwa.

WAKATI Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), ukitarajiwa kufanyika Oktoba 27, mwaka huu, mmoja wa wagombea wa nafasi ya juu kwenye uchaguzu huo, anadaiwa kuwahonga wajumbe wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment