Tuesday 30 July 2013

HAPA NI WAKATI WACHEZAJI WA STARS WAKIJIANDAA KWENDA UGANDA KUPAMBANA NA THE CRANES MECHI YA CHAN


KICHAPO ILICHOKIPATA STARS KUTOKA KWA WAGANDA, CHAZIDI KUWAPASUA VICHWA WAPENZI NA MASHABIKI WA SOKA NCHINI TANZANIA;

·        Wasema Stars haina jipya, ni sawa na ‘maiti’ ile ile ila sanda tofauti

·        Lawama lukuki zaelekezwa kwa TFF

                         Na. deo kaji makomba.

Kipigo ilichokipata timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa stars, kutoka kwa timu ya soka ya taifa ya Uganga The Cranes, cha mabao 3 – 1, wikiend iliyopita huko kwenye uwanja wa Nambole Kampala nchini Uganda kimezidi kuwapasua vichwa wapenzi na mashabiki wa soka nchini, huku wakisema kuwa  bado kuna safari ndefu katika kandandanda la Tanzania.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti na Kisima cha habari, wapenzi na mashabiki wa soka nchini wamesema kuwa bado kuna kazi kubwa kwa soka la Tanzania kutokana na kiwango ilichokionesha Stars jumamosi iliyopita na hivyo kupelekea kuondolewa katika harakati za kuwania tiketi ya kuelekea nchini Afrika ya kusini katika fainali za  CHAN zinazotarajiwa kufanyika hapo mwakani.

Miongoni mwa wapenzi na mashabiki hao aliyezungumza na Kisima cha habari ni John Mwambigija, ambaye amesema kuwa hakuna jipa katika kikosi cha Stars kutokana na kutokuwepo na program endelevu katika soka la Tanzania.

Mwambigija ambaye pia ni muhadhiri katika chuo cha biashara CBE, Campus ya Mwanza amesema, timu ya soka ya taifa ya Tanzania haina jipya, kutokana na shirikisho la soka nchini Tanzania, TFF, kushindwa kuwa na program ya muda mrefu hali inayoifanya timu hiyo kutokuwa na jipya.

“Unajua ndugu mwandishi, hii ni sawa na maiti ileile ila sanda tofauti, yaani wachezaji walewale ambao hawana jipya ila mashindano tofauti.” Alisema Mwambigija.

Aidha Mwambigija ameongeza kusema kuwa lawama za kushindwa kupaa kwa soka la Tanzania zinapaswa kuliangukia TFF, kutokana na shirikisho hilo kushindwa kuzingatia program ya soka la vijana na hivyo Tanzania kushindwa kuzalisha wachezajiwapya na hivyo kubaki na kizazi kilekile.

“Kikowapi kikosi cha Copacoca cola cha Tanzania kilichotisha Brazil takriban miaka saba iliyopita? Alihoji Mwambigija na kuongeza kuwa TFF haikuwa na mpango wowote wa kuwalea wachezaji hao ambao wangekuwa tegemeo kwa badae katika soka la Tanzania.

Shabiki mwingine kuzungumza na Kisima cha habari ni Christian Ndunguru, ambaye yeye amesema kuwa matokeo mabaya ya stars yanatokana na Tanzania kukosa mizizi ya soka hivi sasa.
Ndunguru amesema kuwa kuwa hakuna ukuzaji na  mwendelezo wa vipaji vya soka la Vijana nchini, kiasi kwamba soka la Tanzania kutoboa  itakuwa ni sawa na ndoto za alinacha.

“Hebu angalia mwandishi mashindano kama ya Copa Coca Cola na haya ya Airtel Raising Stars yana malengo mazuri isipokuwa baada ya hapo, wachezaji wanopatikana hawaendelezwi.” Alisema Ndunguru mkazi wa National jijini Mwanza.

Kila mara mipango ya timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, taifa stars, ya kutaka kusonga mbele katika mashindano mbalimbali ya soka imekuwa ikigonga ukutaa, ikiwemo ile safari ya kuelekea nchini Brazil hapo mwakani katika fainali za kombe la dunia, na safari hii ikiondolewa na Uganda katika safari ya kuelekea fainali za CHAN nchini Afrika Kusini hapo mwakani.

Wakati huohuo kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa stars, Kim Poulsen, amesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa kipigo ilichokipata Stars kutoka kwa Waganda na hivyo kuondolewa katika harakati za kuwania tiketi ya kuelekea katika fainali za CHAN nchini Afrika Kusini, hapo mwakani.
Kocha huyo wa Stars ametoa kauli hiyo jumatatu hii mbele ya wandishi wa habari jijini Dare es salaam,  mara baada ya kuwasili kwa kikosi hicho kutokea mjini kampala nchini Uganda, huku Stars ikiiondoshwa katika safari ya kuelekea fainali za CHAN kwa jumla ya mabao 4 – 1 na The Cranes. 
                                        Kim Poulsen, kocha mkuu wa Stars

 Poulsen amesema kuwa licha ya kupoteza nafasi ya kuelekea katika fainali za CHAN, sasa mipango yake anaielekezea katika fainali za michuano ya fainali 2015.

No comments:

Post a Comment