Tuesday 30 July 2013

BARANI ULAYA NA MANDALIZI YA VILABU KUELEKEA MISIMU MIPYA YA LIGI KUU



SEKESEKE LA USAJILI WA  WACHEZAJI WA SOKA  BARANI ULAYA;
·     Dau la paun milioni 85 “lamdatisha” Bale
·     Ataka Spurs wafanye mazungumzo na Madrid
            
         Na. deo kaji makomba.

Mchezaji wa timu ya soka ya Tottenham Spurs ya Englang, Gareth Bale, ameonesha nia yake ya kutaka kuzungumza na klabu ya soka ya Real Madrid ya nchini Uispania ili kuona uwezekano wa kuichezea klabu hiyo, lakini mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy amesema katu mshambuliaji huyo hatouzwa katika Real Madrid.

Madrid tayari walikwishawasilisha mkataba wa kimandishi wakimtaka mshambuliaji huyo,ingawa Spurs imesisitiza kuwa bado mawazo yake ni kuendelea kubaki na na Bale mwenye umri wa miaka 24, licha ya kwamba wamepokea  mkataba mnono uliovunja rekodi ya dunia wa paun million 85.

Tottenham wana matumaini ya kumshawishi Bale kukamilisha mwaka wake mmoja uliosalia katika mkataba wake wa miaka mitatu na timu hiyo ya England.
Bale alijiunga na Spurs akitokea klabu cha soka cha Southampton kwa dau la pauni milioni kumi mnamo mwaka 2007.

Madrid  wanatarajia kuendelea na nia yao katika wiki ijayo na kuwataka Tottenham kumuachia mchezaji huyo ambaye alikwamisha wavuni jumla ya magoli 26 katika mashindano yote msimu uliopita.


 Mshambuliaji wa kimataifa gareth Bale anayeliliwa kwa udi na uvumba na Real Madrid ya Uispania, akiwa katika pozi.

Tottenham ilirejea  mjini London jumapili iliyopita ikitokea katika mandalizi yake ya mwishomwisho ya kindumbwendumbwe cha ligi kuu ya soka ya England huko nchini Hong Kong. Bale hakucheza katika mechi yoyote  katika ziara hiyo barani Asia kutokana na tatizo la msuli.

Mnamo mwezi mei mwaka huu wakala wa Bale, Jonathan Barnett aliiambia televishen ya nchini Uispania mteja wake atafarijika kusikia kutoka kwa rais wa Real Madrid, Florentino Perez.

Kwa Madrid kuendelea na nia yake, kwa upande wa Bale wikiend hii wametoa taarifa muhimu kwa Spurs anahitaji kuwepo na uwezekano wa mazungumzo ya kuondoka kuelekea Uispania.

Ijumaa iliyopita, meneja wa Spurs, Andre Villas- Boas alikataa katakata kujibu maswali kuhusiana na hali iliyopo hivi sasa kuhusiana na mchezaji huyo kutakiwa na Madrid, mbali na kusema kuwa mkataba ndio unaozungumza na wanaendelea na  mshambuliaji huyo ambaye alishinda tuzo ya mchezaji wa kulipwa ya mwaka,  inayotolewa na chama cha soka cha England, FA, pamoja na ile ya mchezaji chipkizi katika msimu uliopita.
                                                             
Bado inaonekana kuwa Bale ataichezea timu yake ya Tottenham katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Monaco ya Ufaransa wikiendi hii, lakini huko uispania, meneja mpya  wa Madrid Carlo Ancelotti anajiandaa na ujio wa mchezaji huyo ambaye akichukuliwa na Madrid atakuwa amevunja rekodi ya kusajiliwa kwa dau kubwa.

Jumamosi iliyopita, Ancelotti alimtoa Cristiano Ronaldo katika upande wa kushoto na kumpa majukumu ya kucheza katikati wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kujiandaa na ligi ya Uispania wakishinda dhidi Paris St-Germain nchini Sweden huku kocha huyo raia wa Uitaliano akijaribu kutafuta mfumo mpya ambao utawajumuisha wote Bale na Ronaldo.

No comments:

Post a Comment