Wednesday 26 June 2013

KUELEKEA LIGI KUU YA SOKA YA ENGLAND.....



PAUNI MILIONI 18 ZAMPLEKA ANDREW SCHURRLE CHELSEA.

·        Sasa kuungana na mjerumani mwenzake, Marko Marin

·        Ni usajili wa kwanza wa Morinho tangu arudi tena Chelsea

     Na. Deo Kaji Makomba

 Barani ulaya klabu ya kandanda ya Chelsea ya Englang, imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa ujerumani Andrew Schurrle, ambaye alikuwa akichezea klabu ya kandanda ya Bayer Liverkusen katika ligi kuu ya soka ujerumani almaarufu Bundedliga kwa dau pauni 18

Schurrle, amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na bosi wa klabu ya Chelsea ya England, Jose Mournho, tangu kocha huyo arejee kwa mara pili katika klabu hiyo iliyoko ligi kuu ya soka ya England, akitokea Real Madrid ya nchini Uispania.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa ujerumani, amemwaga wino kuichezea Chelsea kwa kipindi cha miaka mitano

“Hii ni heshima kwangu kuichezea klabu hii, na timu hii yenye mashabiki wengi.”Alisema Schurrle.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22, aliweza kuifungia magoli 11 katika mechi 34 za ligi kuu ya soka ya Ujerumani timu yake ya liverkesen kati ya mwaka 2012 na 2013.

Katika michezo hiyo aliyocheza, iliweza kuisaidia klabu yake ya Liverkusen kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu.

Schurrle, ambaye hucheza nafasi ya pembeni au wakati mwingine hucheza kama mshambuliaji wa kati, amefunga mabao saba katika mechi 24 akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani na alikuwemo katika cha timu hiyo katika michuano ya Euro 2012.

Scherrle, anaungana na mjerumani mwenzake Marko Marin, ambaye alielekea Stamford Bridge akitokea  Werder Bremen mwezi Julai mwaka 2012, lakini alicheza mechi 12 katika msimu wake wa kwanza.

No comments:

Post a Comment