Wednesday 26 June 2013

KIDUMBWENDUMWE CHA KOMBE LA MABARA HUKO BRAZIL..



NUSU FAINALI YA KWANZA KUPIGWA LEO USIKU, NI BRAZIL NA URUGUAY, SPAIN NA ITARIA ALHAMIS HII.

Na.Deo Kaji makomba.

Harakati za kuwania kombe la mabara almaarufu kama Confedaration Cup, zinazidi kushika kasi huko nchini Brazil, huku timu zitakazocheza hatua ya nusu fainali ya mahindano hayo tayari zikiwa zimejulikana.
Timu hizo ni Brazil, Uruguay, Uispania pamoja na Italia.

Brazil ilifanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuongoza kwa kuwa na pointi tisa kibindoni katika msimamo wa kundi A wakati Italia nayo imweza kuingia hatua hiyo ikimaliza hatua ya makundi kwa kuwa na pointi sita.

Nalo kundi B lilimaliza hatua yake ya makundi huku Uispania ikiongoza katika kundi hilo kwa kuwa na pointi tisa na Uruguay ikimaliza hatua hiyo kwa kuwa na pointi sita.

Mechi ya nusu fainali ya kwanza ya mashindano hayo, inazikutanisha Brazil na Uruguay, mechi itakayopigwa kuanzia saa mbili usiku kwa saa za Afrika mashariki.

Nayo nusu fainali ya pili itapigwa alhamis hii, ambapo Uispania itakuwa ikioneshana kazi na Italy.

Ufuatao ni msimamo vile ulivyo baada ya kumalizika kwa mechi hizo za hatua ya makundi ya mashindano hayo ya kombe la mabara ama Confedaration Cup.

Group A
Team
MP
W
D
L
GF
GA
Pts
3
3
0
0
9
2
9
3
2
0
1
8
8
6
3
1
0
2
3
5
3
3
0
0
3
4
9
0


Group B
Team
MP
W
D
L
GF
GA
Pts
3
3
0
0
15
1
9
3
2
0
1
11
3
6
3
1
0
2
7
6
3
3
0
0
3
1
24
0






No comments:

Post a Comment