Saturday 21 December 2013

YANGA MDEBWEDO HAINA JIPYA. YAGEUZWA KAMA CHAPATI NA SIMBA KATIKA MECHI YA NANI MTANI JEMBE. >>>>>>>>>

Kikosi cha timu ya Simba kikiwa kimepozi katika picha ya pamoja na kikombe chao cha nani mtani jembe.


Yanga haina jipya kabisa.
·    Yageuzwa kama chapatti uwanja wa Taifa.
·    Yakubali kichapo cha mabao 3 - 1      kutoka kwa Simba.
·    Ilikuwa ni katika mechi ya nani mtani jembe?

 Na. Mwandishi wetu Dar.

Timu ya soka ya Simba ya jijini Dar es salaam, leo imewadhihirihisha wapenzi na mashabiki wake kuwa timu ya soka ya Yanga ya Dar es salaam si lolote, baaada ya kuwafunga watani wao wa jadi Yanga mabao 3 - 1.  
Mchezo huo ulikuwa ni wa kumtafuta mtani nani jembe ulifanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku wekundu wa Msimbazi Simba wakionekana kutawala mchezo huo ulidhaminiwa na bia ya Kilimanjaro.
 Mlinda mlango wa timu ya Simba Ivo Mapunda akiokoa hatari langoni mwake, wakati wa mchezo huo wa nani mtani jembe, uliopigwa katika uwanja wa taifa.

 Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi huku Simba wakionana vyema na kuwanyanyasa wachezaji wa Yanga, ambao walionekana kuelemewa hususani sehemu ya kiuongo na hivyo kuonekana kama vile hawamo uwanjani huku Simba wakiendelea kutakata na kufanya vitu vyao.

Ilikuwa ni katika dakika ya 19 ya mchezo  pale Wekundu wa Msimbazi  Simba walipoandika bao la kwanza likifungwa na Hamis Tambwe, baada ya mabeki wa Yanga kuzubaa na hivyo mchezaji huyo kufunga bao hilo.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia timu yao wakati ikiinyosha Yanga katika mechi ya nani mtani jembe. Picha ikimuonesha shabiki mmoja wa Simba ambaye jina lake halikuweza kufahamika huku wazimu ukiwa umempanda akivua nguo na kubaki katika chupi.


Hamis Tambwe kwa mara nyingine aliiandikia bao la pili timu yake ya Simba kwa mkwaju wa penaiti kunako dakika ya 43, penaiti iliyopatikana baada ya kiungo wa Simba Singano kuangushwa katika eneo la hatari.
 Kipigo kinaumiza. Shabiki wa timu ya Yanga akionekana hana raha baada ya kuonekana timu yake mdebwedo mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 3 -1


Hadi mapumziko Simba walikuwa wakiongoza kwa mabao 2 – 0, wakati Yanga walikuwa hawajapata kitu.
Bao la tatu la Simba lilifungwa na mchezaji Awadhi.

Yanga walipta bao la kufutia machozi kwa upande wa Yanga lilifungwa Emmanuel Okwi, na hadi mwisho wa mchezo Simba 3  Yanga 1.
Simba imeweza kujinyakulia hundi ya shilingi 100,000,000 kama washindi katika mchezo huo wa nani mtani jembe.


No comments:

Post a Comment