Saturday 21 December 2013

KAGASHEKI ABWAGA MANYANGA KATIKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

Aliyekuwa Waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamisi Sued Kagasheki, ambaye ametangaza kujiuzulu.


Balozi Kagasheki atangaza kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri.
·    Ni uwaziri wa maliasili na utalii
·    Ripoti ya kamati ya Ardhi, Maliasili na mazingira yamkuta na hatia ya uzembe.
·    Kuhusiana na sakata la operesheni tokomeza ujangili.

Na. Mwandishi wetu.

Waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamisi Kagasheki, ametangaza nia ya kujiuzulu wadhifa huo ikiwa ni muda mfupi uliopita huko bungeni mjini Dodoma.

Sababu kubwa ya kujiuzulu ni baada ya kusomwa ripoti ya kamati ya Ardhi, Maliasili na mazingira, ikimtuhumu kuzembea na kukithiri kwa vitendo viovu vilivyofanywa na wanausalama wakati wa operesheni ya tokomeza ujangili.

Kwa mujibu wa ripoti ya kamati hiyo, imebainisha kuwa operesheni hiyo tokomeza ujangili iliyoendeshwa na serikali ilikuwa na unyanyasaji mkubwa  wa wananchi , ukatili, udharirishaji, ubakaji na mauaji huku baadhi ya wazazi wakivuliwa nguo, kuteswa na kubakwa mbele ya familia.

Akiwakilisha taarifa ya kamati hiyo, mwenyekiti wake James Lembeli, amesema kuwa pamoja na mates o hayo yaliyowakumba wananchi pia nyumba zao zilichomwa na mifugo kupigwa risasi huku mingine ikifa kwa kukosa maji, chakula na maziwa kwa ndama wadogo.

Kamati hiyo pia imebainisha kuwepo kwa vitendo vya Rushwa vilivyotawala operesheni hiyo, ambapo pia wananchi waliokuwa na mifugo walitozwa faini na mifugo mingine kuuzwa kwa bei nafuu ambayo haikulingana na faini iliyokuwa ikitoza na wafugaji walizuiliwa kushiriki katika mnada wa uuzaji wa mifugo hiyo.

No comments:

Post a Comment