Sunday 15 December 2013

TATA MADIBA AZIKWA KWA HESHIMA ZOTE BILA KUSAHAU MILA NA DESTURI.



Mandela azikwa kijijini kwao huko Qunu Afrika Kusini.
·    Takribani watu 4,500 wahudhuria mazishi.
·    Azikwa kwa heshima zote, huku mila na desturi za kabila lake zikizingatiwa.

Na. Mwandishi wetu.

Mazishi ya Nelson Mandela yamefanyika leo jumapili katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja baada  ya maombolezi ya shujaa wa Afrika marehemu  Nelson Mandela.

Takriban watu 4,500 ikiwemo wageni wa kimataifa wamehudhuria mazishi hayo ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa.

Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale na pia wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa.
 Jeneza la aliyekuwa rais wa kwanza mweusi, Tata Nelson Mandela likisindikizwa na makamanda wa juu wa vikosi vya usalama, wakati wa mazishi yake huko Qunu, Afrika ya kusini.


 Ni kuambatana na tamaduni na mila za watu wa ukoo wa Mandela wa Thembu.

Viongozi wa Afrika, familia na marafiki wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati Nelson Mandela katika mazishi yake ya kitaifa katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Cape Mashariki. Mandela alikuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini.

Rais Jacob Zuma alisema kuwa wakati safari ndefu ya Mandela kuelekea uhuru imekwisha, raia wa Afrika Kusini wana jukumu la kuendeleza sera zake na urithi wake.

No comments:

Post a Comment