Aliyekuwa mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoa wa Mwanza marehemu, Clement Mabina,ambaye ameuwawa kwa kushambuliwa na wananchi wa kanyama Kisesa.
Aliyekuwamwenyekitiwa zamani wa CCM
Mkoani Mwanza, auwawa.
·
Ni Clement
Mabina.
·
Ashambuliwa
na wananchi wenye hasira.
·
Kisa
chaelezwa ni ugomvi wa mashamba.
Na. Mwandishi wetu.
MWENYEKITI wa zamani wa chama cha mapinduzi(ccm) mkoa wa Mwanza
Clement Mabina ambaye pia ni diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani
Mwanza ameuawa na wananchi wenye hasira katika ugomvi wa mashamba.
Tukio la kuuawa kwa Mwenyekiti huyo
wa Ccm Mkoa wa Mwanza ambaye alishindwa katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti
wa ccm mkoa wa Mwanza mwaka jana na Waziri wa zamani na Mbunge wa zamani wa
Ilemela Dk Antony Diallo lilitokea leo asubuhi katika eneo la kijiji cha
Kanyama wilayani Magu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana
na kuthibitishwa na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD) ya Magu ODC Mkapa pamoja na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga zimeeleza kuwa
tukio limetokea majira ya saa mbili asubuhi.
ODC Mkapa alikiri kutokea kwa tukio
la kupigwa na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Ccm Mkoa na Mwenyekiti wa
zamani wa Halmashauri ya wilaya ya Magu baada ya kutokea kutokuelewana baina
yake na wananchi wa eneo la kijiji cha Kanyama alikokuwa na shamba lake
alikokuwa amekwenda kupanda miti.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Magu Desdery Kiswaga alisema kuwa amepokea taarifa za kuuawa kwa
kupigwa na wananchi wenye hasira kutokana na ugomvi wa mashamba na kuelezwa
kuwa amesikitishwa sana na kuuawa kwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa Halmashauri
ya wilaya ya Magu.
Taarifa zaidi toka eneo la tukio la
Kanyama kulikotokea mauaji hayo zimeeleza kuwa Mwenyekiti huyo wa zamani wa CCM
alifika katika eneo hilo majira ya asubuhi kwa ajili ya kupanda miti katika
eneo la milima ya Kanyama ambalo analimiliki ambavyo hata hivyo linadaiwa kuwa
na mgogoro baina yake na wananchi.
Baada ya kufika katika eneo
hilo,wananchi nao walifika katika eneo hilo na kumhoji sababu za kupanda miti
katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro wa umiliki na kutokea kutokuelewana
baina yake na wananchi.
Baada ya majibishano ya muda mrefu
na kuona wananchi wameanza kumzingira Mabina aliamua kufyatua risasi hewani
kuwatawanya wananchi hao ambapo kwa bahati mbaya mojawapo ya risasi hizo
zilimpiga mtoto aliyekuwa katika eneo hilo na kupoteza maisha.
Taarifa hizo toka katika eneo hilo
la tukio zimeeleza kuwa kutokana na tukio hilo wananchi walimzingira Mabina na
kuanza kumpiga kwa silaha mbalimbali za jadi kama vile mapanga, fimbo, mawe,
mikuki na kusababisha kifo chake papo hapo.
Kabla ya kurejea chama cha
mapinduzi(ccm) na kufanikiwa kuwa diwani wa Kata ya Kisesa na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mabina aliwahi kuwa mwanachama wa chama cha
NCCR-Mageuzi na aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo mwaka 1995 na
kushindwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Malaki Lupondije.
No comments:
Post a Comment