Wednesday 4 December 2013

MAHAKAMA SI RAFIKI KWA WATOTO NCHINI TANZANIA.




Mahakama si rafiki kwa watoto nchini Tanzania.

·    Zadaiwa kutozifahamu sheria na haki za watoto.
·    Zaelezwa kuwafunga watoto kwa kuwachanganya na watu wazima magerezani.

                                                          Na. Baltazar Mashaka.

MAHAKAMA nchini zinadaiwa si rafiki wa watoto na hazifahamu haki na sheria zao,hali inayochangia waharibike wanapotiwa hatiani na kufungwa pamoja na watu wazima magerezani.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni Jijini Mwanza na Loata Lomitu,mtaalamu wa masuala ya watoto kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wakati akitoa mada kwenye kongamano la Malezi,Makuzi na Maendleo ya awali ya Mtoto (MMMAM),lililoandaliwa Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Home Economic Association (TAHEA)

Alisema watoto wanapofikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali na kutiwa hatiani, hufungwa pamoja na watu wazima katika magereza bila kuzingatia ummri wao, sheria na haki zao pamoja na ulinzi.

Alisema watoto hao wanapofungwa magerezani, huchanganywa na watu wazima ambao huwafanyia vitendo vya ukatili kwa kuingiliwa (kulawitiwa), hali inayowafanya waharibike na kuathirika kisaikolojia .

“Mahakama zetu bado si rafiki kwa watoto na hazifahamu haki na sheria za watoto, hata wakifungwa wakitoka wanarejea tena huko sababu wameharibika! Wanatakiwa wapelekwe kwenye shule za maadili badala ya magereza,”alisema Lomitu

Kuhusu ulinzi wa mtoto Lomitu alisema, huanzia tangu akiwa tumboni na baada ya kuzaliwa anakuwa kiakili, kimwili na kijamii na kupata stadi za maisha,hivyo jukumu la ulinzi ni la wadau wote kwani yapo madhara makubwa kuuawa kwa watoto wengi.

Alisema baadhi ya wazazi wanachangia watoto wao kuharibika sababu ya kutafuta mahitaji ya familia na kuonya wanaopeleka watoto wadogo katika shule za bweni, kuwa huko si kumlinda na hakuna matunzo wala malezi mazuri.

Hata hivyo alidai lipo ongezeko kubwa la ukatili wa watoto na watoto waanaoishi kwnye mazngira hatarishi (mitaani) kuw chanzo chake ni mgogoro ya ndooa katika baadhi ya familia.

Kwamba matunzo na malezi kwa watoto katika baadhi ya familia si mazuri kwa sababu ya ubinafsi na ubaguzi kati ya watoto wa kike,ambapo wa kiume wanaonekana bora,hali ambayo inachangia kuwepo kwa matabaka.

“ Mafisadi tunawazalisha sisi wenyewe kutokana na malezi  na makuzi ya watoto.Lakini pia upo ubaguzi kwa watoto wa kike,wanapewa kazi nyingi majumbani aambao husababisha washindwe kufaulu vizuri mitihani.Huko ni kuzalisha matabaka kwa kuwaona waatoto wa kiume ni bora kuliko wa kike,”alisema Lomitu

Alidai kwamba vitendo vya ukatili kama ubakaji,vipigo,ndoa zenye migogoro na baadhi ya majina kama Shida,Matatizo na Taabu, yanachangia kuharibu maisha ya watoto na kuwapoteza.


Alisema ni vema jamii ikarejea malezi ya zamani kwa kila mtu kuangalia jinsi ya kuwalea watoto na kutowapa uhuru mkubwa ili kujenga kizazi chenye maadili mazuri.
Kama taifa tuanze upya na tuwasaidie walimu kutengeneza zana za stadi za watoto kujifunzia na kufundishia , tuaanzee na malezi na makuzi,badala ya kubaki tunazodoana,hilo halitatusaidia

No comments:

Post a Comment