Sunday 17 November 2013

ZAO LA PAMABA NA DAWA ZA VIUWADUDU BANDIA.

Waziri wa chakula kilimo na ushirika, Eng. Christopher Chiza.
Katika kuimarisha zao la Pamba kwa wakulima.
·    Serikali kuwachukulia hatua kali watakaoingiza dawa bandia za viuadudu.
·    Dawa hizo zadaiwa kutokuwa na ujazo sahihi.
                                             
                                     Na. Mashaka Bartazal.

SERIKALI imesema itawachukulia hatua za kisheria waingizaji na wasambazaji wa dawa za viuadudu watakaoingiza nchini dawa bandia na zenye ujazo usiostahili za zao la pamba.

Pia serikali imesema itawachukulia hatua kali za kisheria, mawakala na wasambazaji pembejeo na  dawa za viuadudu vya zao hilo, wataochakachua na kuingiza dawa bandia nchini pamoja na kuharibu mizani kwa nia ya kuwaibia wakulima.

Onyo hilo lilitolewa jana na Waziri wa Chakula,Kilimo na Ushirika, Christopher Chiza,wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwandu katika wilaya ya Kwimba, mkoani  Mwanza.

Waziri Chiza alitoa onyo hilo baada ya Mbunge wa Jimbo la Sumve wilayani Kwimba, Richard Ndassa kudai mbele ya waziri kuwa wasambazaji wa dawa za viuadudu vya zao la pamba wanawasambazia wakulima  wa zao hilo dawa bandia na zenye ujazo mdogo.

Ndassa alisema dawa hizo zinzosambazwa jimboni mwake, hazina uwezo wa kuuwa wadudu waharibifu wa zao hilo na kudai huko ni kuwaibia wakulima.

“Ndugu waziri  jimboni kwangu tunaletewa dawa  bandia za kuulia wadudu waharibifu wa zao la pamba. Madawa hayo hayawezi kuuwa wadudu,huko ni kuwaibia wakulima,”alisema Ndassa.

Pia alimweleza waziri huyo wa Kilimo,Chakula na Ushirika kuwa hata mizani ya kupimia uzito wa pamba nayo inawaibia mno wakulima hao ,hal inayosababisha washindwe kunenepa.

“Mheshimiwa Waziri watu hawa wanawaibia wakulima kwenye mbegu,viuadudu na kwenye mizani,kwa mtindo huo wakulima hawawezi kunenepa. Wasambazaji dawa na wanunuzi wa pamba watusaidie leo, wako hapa,” alisema mbunge huyo wa Sumve

Kutokana na kauli ya mbunge huyo Waziri Chiza alisema serikali itakuwa macho kufanya ukaguzi kwa waingizaji wa dawa hizo na kuwachukulia hatua za kisheria.

Chiza alidai kuwa aliyesambaza dawa za hizo zenye kasoro atasaidia kuonyesha aliyeziingiza, na wote kwa pamoja watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kuwaeleza wananchi kuwa, wakaguzi na vyombo vyake wapo, hivyo wakulima wasaidie kuwafichua wachakachuaji wa viuadudu.

“Mwaka jana tatizo la dawa bandia lilionekana tukalivalia njuga ikiwa ni pamoja na TPRi. Walingizaa dawa katika ujazo usiostahili.Serikali tutakuwa macho kwa kufanya ukaguzi kwa waingizaji na wasambazaji,sababu haazitawsaidia wakulima,”alisema

Kwa upande wa bei yaa pamba msimu huu alisema bei dira ilikuwa sh.700 kwa kilo moja lakini wakulima wameuza hadii sh.1000 kwa kilo moja.

Chiza aliwaonya wakulima kutokubali kurubuniwa na wanunuzi katika upangaji wa bei,kwani wawakilishi wanaotumwa badala ya kuwapigania wanashirikiana na wanunuzi kushusha bei kwa maslahi yao.

No comments:

Post a Comment