Rais mpya wa TFF, Jamali Malinzi
TFF YATAKA ORODHA YA WALIOSAMEHEWA.
·
Ni kufuatia msamaha wa rais mpya wa shirikisho
hilo.
·
Vyama vya soka ngazi ya wilaya, mkoa na vyama
shiriki kuwajibika katika hilo.
Na. Mwandishi wetu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limevitumia waraka vyama vya mpira
wa miguu vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuvitaka kuwasilisha orodha ya wote
waliofaidika na msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.
Taarifa hiyo ya TFF kuvitumia waraka
vyama vya soka vya wilaya, mikoa na vyama shiriki kuhusiana kutaka orodha ya
waliosamehewa katika msamaha wa rais wa TFF, imetolewa na kaimu katibu mkuu wa
shirikisho hilo, Boniphace Wambura.
Oktoba 28 mwaka huu wakati akizungumza
katika Mkutano Mkuu mara baada ya
kumalizika kwa uchaguzi wa shirikisho la soka nchini Tanzania, TFF, Rais mpya
wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi alitoa msamaha kwa wote waliofungiwa kwa
sababu mbalimbali.
Taarifa hiyo iliyotolewa na TFF,
imesisitiza kuwa, msamaha huo hauwahusu waliofungiwa kutokana na makosa ya
rushwa au kupanga matokeo. Vilevile
haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.
Vyama vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha
waraka huo unafika kwa wanachama wao (vyama vya mpira wa miguu vya wilaya). TFF
inataka orodha ya wote waliofaidika na msamaha huo kwa ajili ya kumbukumbu zake
(records).
No comments:
Post a Comment