Mmoja wa watu akijitolea damu kwa ajili ya kuchangia benki ya damu kusaidia watu wanaokuwa na mahitaji ya huduma wakati wanapokuwa wamepungukiwa damu.
Chupa 40,000 za damu zahitajika.
· Ni katika kituo cha taifa cha mpango wa damu salama kanda ya
ziwa.
· Lengo ni kukabiliana na upungufu wa damu katika hospitali
kanda ya ziwa.
Na. Mashaka
Bartazal.
KITUO cha Taifa cha Mpango wa Damu Salama, Kanda ya Ziwa,
kinahitaji chupa 40,000 za damu ili kukabiliana na upungufu wa damu
kuweza kuhudumia hospitali za mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Upungufu huo ulibainishwa jana Jijini Mwanza na Ofisa
Mhamasishaji wa Mpango wa Damu Salama Kanda ya Ziwa, Vincent Muhada,
akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiari, lililoandaliwa
na Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania.
Alisema, mahitaji halisi ya damu salama kwa mikoa ya Kanda
ya Ziwa ni chupa 70,000, lakini hadi sasa chupa zinazopatikana ni kati ya
25,000 hadi 30,000 , hivyo kuwa na upungufu wa chupa 40,000.
Muhada, tatizo la upungufu wa damu salama linasababishwa na
jamii yenyewe kutoshiriki kikamilifu kujitolea kwa hiari kuchangia damu kwa
ajili ya kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo hospitalini.
Alisema Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania
inastajhili kupongezwa kutokana na moyo wa kujitolea kuchangia damu
salama,kwani hali itasaidia jamii na wagonjwa waliolazwa hospitalini
kupata mahitaji ya damu.
“Niipongeze taasisi hihi kwa kuchangia damu ili kuokoa
maisha ya watu wengine wenye mahitaji ya damu.Mahitajii halisi ya damu, ni
chupa 70,000 kwa mwaka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Lakini hadi sasa tuna
chupa 25,000 hadi 30,000 tu! Tatizo laupungufu huo linatokana na wananchi
kuogopa kujitolea kuchangia damu,” Muhada.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Bilal Muslim
Mission of Tanzania, Sibtain Meghji, aliitaka jamii kujitolea kwa moyo mmoja
kuchangia damu, kwani hiyo itasaidia sana kuokoa wagonjwa wenye kuhitaji damu
waliopo hospitalini na wananchi wanaohitaji huduma hiyo.
Alisema kila mwaka taasisi hiyo kwa kushirikiana na
waumini wote wa madhehebu ya Shia Ithna Asheri, wamekuwa wakiendesha mpango huo
wa kuchangia damu, na zoezi hilo jana lilitarajiwa kukusanya zaidi ya chupa 400
kutokana na idadi ya watu waliojitokeza.
“Taasisi yetu imekuwa mstari wa mbele kuhamasisha
waumini wa dini ya madhehebu ya Shia na jamii kujitolea kuchangia damu
kwa ajili ya watu wenye matatizo.,” alisisitiza Meghji.
Aidha, Meghji aliviomba vyombo vya dola kutekeleza vema
majukumu yake kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaohujumu kwa
kuuza damu hospitalini, na kuiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuchangia damu
punde zoezi hilo linapofanyika.
Mmoja wa watu wa kwanza waliojitolea kutoa damu katika zoezi
hilo, Hussein Shaban, aliwaambia waandishi wa habari kwamba: “Kila mwaka mimi
lazima nitoe damu kwa ajili ya binadamu wenzangu wanaohitaji damu hospitalini.
Na naomba sana watu wengine wajitolee ili tuokoe maisha ya ndugu zetu, maana
binadamu wote ni sawa”.
Kituo cha Taifa cha Damu Salama Kaya Ziwa kinahudumia
hospitali zote za mikoa ya Mwanza,Mara,Kagera,Shinyanga,Geita,Tabora na Kigoma
No comments:
Post a Comment