Sunday 6 October 2013

MASKINI TOTO AFRICAN JENGO LAKE KUPIGWA MNADA!

Jengo la klabu ya Toto African ambalo linatakiwa lipigwe mnda ili kufidia deni la mkopo wa sh.13 milioni.Jengo hili liko katika mitaa ya Bantu na Kishamapanda.(Picha na Mashaka Baltazar)

Jengo la timu ya Toto African ya Mwanza kuuzwa.

  •     Kulipa deni la hilingi milioni 13 wanazodaiwa.

  •     Uongozi wa timu hiyo wasema, ni njama za kutaka kuliuza.

                        
                          Na. mashaka baltazar, Mwanza.
WAKATI timu ya Toto African,ikikabiliwa na ukata wa fedha na kutokuwa na uongozi wa kudumu, kuna habari za kutaka kuuzwa kwa jengo la klabu hiyo.

Toto inamiliki jengo moja lililopo katika makutano ya mitaa ya Bantu na Kishamapanda, katikati ya Jiji la Mwanza,ambalo sasa linataka kuuzwa ili kulipa mkopo wa sh. 13 milioni .

Fedha hizo zilikopwa na uongozi wa klabu hiyo, kwa ahadi ya kuzirejesha mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu msimu uliopita,baada ya kulipwa fedha zao na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom .

Akizungumza na Kisima cha habari, msemaji wa klabu hiyo Omar Mbalamwezi,aliseam anasikitishwa kuona wajanja wachache wanataka kuuza mali ya jamii.

Alidai haiwezekani jengo hilo ambalo thamani yake ni zaidi ya sh. 200 milioni likauzwa ili kufidia mkopo wa milioni 13,ukizingatia  wajanja wameongeza kiasi kingine cha sh.3 milioni bila sababu na huu ni wizi wa mchana.

“Baadhi ya watu wamekuwa madalali wanataka kuuza jengo la klabu kwa sh.13 milioni ambazo tulikopeshwa na mdau mmoja bila riba,leo wao wameback date na kuongeza deni sasa limefikia sh. 18 milioni na tayari wamepata wanunuzi kwa bei y ash 200 milioni,”alisma Mbalamwezi

Alieleza kuwa anachofahamu kabla ya hatua hiyo,walikutana na mdai wakakubaliana akate fedha hizo kutoka kwa wapangaji wa jengo hilo hadi deni lake la sh.13 milioni liishe,  lakini anashangazwa kuona makubaliano yanakuwa kinyume.

“Kwa mfumo tulio nao Katibu wa klabu ni mwajiriwa na jengo ni mali ya jamii hata kama ni la klabu, bado ni ya jamii, hivyo haliwezi kuuzwa kwa deni la sh.13 milioni,”alisema

Msemaji huyo alidai kuwa kutofanyika kwa mambo mbalimbali na uongozi kumaliza muda wake, kunaifanya timu hiyo iikose misaada kutoka kwa watu wenye mapenzi na maendeleo ya mpira.

“Uongozi umemaliza muda wake,wanachama hawana taarifa ya mapato na matumizi,hakuna mkutano uliyoitishwa kuwaeleza kilichosababisha tmu kusahuka na taarifa ya msimu mzima.Yote hayo hayajafanyika na watu wanaotaka maendeleo ya soka hawapendi hivyo,”alisema Mbalamwezi

Alidai kutokana na klabu hiyo kutokuwa na uongozi wa kudumu baada ya kushindwa kufanya uchaguzi kwa kutumia katiba ya zamani, wamekubaliana waikabidhi timu kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, ateuwe uongozi wa muda.

Alisema wameshindwa kukabidhi mzigo wa vifaa hivyo vyenye thamani ya sh. 50 milioni kwa kukosa uongozi wa kusimamia rasilimali hiyo ambayo itainufaisha klabu yao.

Mbalamwezi alisema uongozi wa muda utakaoteuliwa,  utasimamia rasilimali za klabu hiyo pamoja na mradi wa kuuza vifaa vya michezo,kutokana na kusaini mkataba wa miaka 10 wa uwakala wa kampuni ya Insegere Sports ya Marekani .

“Rasilimali tayari zipo,lakini unamkabidhi nani asimamie kuuza mzigo huo wakati huna uongozi.Tumeshindwa kuchagua viongozi sababu watu wanadai katiba mpya.Hivyo bora tukabidhi timu kwa DC tukisubiri uchaguzi,”alisema Mbalamwezi

No comments:

Post a Comment