Rais mpya wa shirikisho la soka nchini Tanzania, TFF, Jamali Malinzi.
Malinzi ndiye
rais mpya wa TFF.
- Atoa msamaha kwa waliokuwa wamefungiwa katika masuala ya soka.
- Nafasi ya ujumbe kwa kanda ya ziwa, Nyalla nje, Lufano ndani.
Na. Mwandishi wetu.
Jamal
Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF
uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Aliibuka
na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani
aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia
aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari
Madega akipata kura sita.
Akizungumza
mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau
wote akiwemo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini
unasonga mbele.
Rais wa TFF aliyemaliza muda wake Leodiga Chila Tenga, akimkabidhi mpira rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi mpira baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa TFF jumapili iliyopita
Rais mpya wa TFF, Jamali Malinzi akiwa na kamati kuu mpya tendaji ya shirikisho hilo.
Pia
ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya,
mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au
kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi
ya klabu.
Rais
Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana
na Kamati ya Utendaji.
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda
namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda
namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya
Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39).
Epaphra
Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya
Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley
Mbise (51), Ally Mtumwa (19).
Kanda
namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi
ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.
Ayubu
Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa
kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye
mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David
Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46).
Kanda
namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura
93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe
Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis
Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11).
Hussein
Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63
akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange
ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto
(26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2).
Kanda
namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka
kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba
13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said
Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex Crispine Kamuzelya (4).
No comments:
Post a Comment