Kamanda wa polisi mkoani mwanza, Bwana Ernest Mangu, akizungumza na Kisima cha habari ofisini kwake jijini Mwanza.(Picha na Deo Kaji Makomba)
Baada ya polisi kupambana
na kuyaua majambazi matatu
yaliyokuwa na silaha jijini Mwanza;
Baada ya polisi kupambana
na kuyaua majambazi matatu
yaliyokuwa na silaha jijini Mwanza;
- Safari hii yakamata meno ya tembo.
- Yalikuwa yamefungwa kwenye gunia la
mkaa ili “kuwazuga” polisi.
Na. deo kaji makomba
Katika kuhakikisha linafanya kweli
kwenye harakati zake za kupambana na matukio ya kiarifu, jeshi la polisi mkoani
Mwanza, limekamata nyara za serikali zilizokuwa zikisafirishwa kutoka mkoani
Mara na hatimaye kukamatwa jijini Mwanza.
Nyara hizo za serikali ni meno ya
tembo ambayo yalikamatwa na asikari polisi waliokuwa katika doria jumatano hii
katika kituo kikuu cha mabasi cha Buzuruga jijini Mwanza.
Tukio hilo la kukamatwa kwa nyara
hizo za serikali jijini Mwanza jumatano hii, limetokea siku chache tu, mara
baada ya jeshi hilo la polisi mkoani Mwanza kupambana kwa kufyatuliana risasi
na majambazi yaliyokuwa na silaha aina ya sub machine gun (SMG) yakiwa katika
harakati za kutaka kupora na kufanikiwa kuyauwa.
Akizungumza na kisima cha habari
jijini Mwanza, kamanda wa polisi mkoani humo Bwana Erenest Mangu, amesema kuwa,
tukio la kukamatwa kwa meno hayo ya tembo, lilitokea majira ya saa tatu na robo
asubuhi.
Kulingana na kamanda Mangu, mnamo
majira hayo ya saa tatu asubuhi, alikamatwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la
Yohana Jackson Charles (27) mkazi wa Butiama mkoani Mara, akiwa na vipande kumi
vya meno ya tembo.
Kamanda Mangu ameongeza kuwa meno
hayo ya tembo yalipopimwa uzito wake umefikia kilo 26, yakiwa na thamani ya shilingi milioni ishirini na
tatu laki mbili.
Meno hayo ya tembo yalikuwa
yamefungwa kwenye junia la mkaa ili “kuwazuga” kama si kuwahadaa watu wa
usalama kama anavyoelezea kamanda Mangu wakati akizungumza na Kisima cha habari
ofisini kwake jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment