Friday 6 December 2013

TANZANIA YAUNGANA NA MATAIFA MENGINE DUNIANI KUOMBOLEZA KIFO CHA MZEE WA MANDELA.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.


Tanzania yatangaza siku tatu za maombolezo.
·    Ni kufuatia kifo cha rais mstaafu wa Afrika ya kusini mzee Mandela.
·    Rais Kikwete asema mfano wa Mandela wapaswa kuigwa.
·    Kenyata awataka watu waige uelewa wa kusamehe bila masharti wale wanaokuwa wamekosa.


Na. Mwandishi wetu.

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ametangaza siku tatu za maombolezi, kufuatia kifo cha mzee Nelsomn Mandela, akisema kua Afrika na dunia nzima kwa ujumla imempoteza shujaa mkubwa sana katika karne ya 20 na 21.

Kikwete alisema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kua Mandela ni kiongozi wa kipekee na mtu aliyeenziwa sana na dunia nzima pamoja na watu wa Afrika Kusini baada ya kupigania sana demokrasia nchini Afrika Kusini.

Kikwete alisema mfano wa Mandela unapaswa kuigwa na watu wote duniani .

Kwa upande wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amesema kuwa Mandela alikuwa mfano mzuri wa umuhimu wa kuwa na matumaini na kuwataka watu kuwa na uelewa wa kuwasamehe bila masharti wale wote wanaotukuosea.

Naye Rais wa Rwanda Paul Kagame,amesema kua Mandela ataendelea kuishi kwenye mioyo ya wengi wetu.

Naye Rais mstaafu Daniel Moi ambaye alikuwa madarakani wakati Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amempongeza Mandela kwa kuhakikisha utulivu wa kisiasa barani Afrika na kuwa mfano bora kwa viongozi wengine.

Naye Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema kuwa Mzee Mandela, pamoja na washirika wake, Albert Luthuli, Walter Sisulu, Govan Mbeki, Oliver Thambo na wengine wengi,walijitolea maisha yao kuleta demokrasia nchini Afrika Kusini. 

Walifanya kila walichoweza kuhakikisha kwa wanawakomboa watu wa taifa lao. 

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Museveni amesema ni jukumu la vijana sasa kuiga mfano wa Mandela kuhakikisha kuwa Afrika inalindwa dhidi ya ukoloni mambo leo na kutengwa.

No comments:

Post a Comment