Sunday 2 March 2014

RIPOTI YA JAJI WARIOBA KUHUSU RASIMU MPYA YA KATIBA YAENDELEA KUPONDWA >>>>>>>

   Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Rasimu ya Katiba Mpya Jaji Joseph Sinde Warioba



Licha ya tume ya mabadiliko ya rasimu mpya ya katiba nchini Tanzania kukamilisha kazi yake,
bado yaendelea kukosolewa -Bituro
·    Yaelezwa maoni yaliyokusanywa yanamapungufu makubwa.
·    Idadi ya waliotoa maoni hakidhi na haiwezi kuwakilisha watanzania milioni 45.

Na. Deo Kaji Makomba.

Wakati  wajumbe wa bunge maalum la katiba wakiendelea na mkutano wa utungaji kanuni alkadharika majadiliano kuhusu rasimu ya katiba mpya iliyoandaliwa na tume maalum ya katiba iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake jaji Joseph Sinde Warioba, wananchi  mbalimbali wamezidi kuikosoa rasimu ya katiba.

Kwa mujibu wa taarifa ya uchambuzi wa takwimu za maoni ya wananchi ya rasimu ya katiba mpya uliofanywa  na Paschal Bitulo Kazeri  ambaye ni mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii na nakala yake kukifikia Kisima chetu  cha habari, imeeleza kuwa,  nia ama malengo ya kufanya mabadiliko ya katiba mpya ni mazuri kwani katiba iliyopo ama kwa hakika imepitwa na wakati na hivyo kutokwendana na wakati wa sasa.

Katika taarifa yake hiyo ya uchambuzi, Bituro ameleza kuwa licha ya tume ya jaji wariomba kumaliza kazi yake, imeonesha mapungufu makubwa na kwamba haiakisi maoni na na takwimu za maoni ya watanzania.
Kulingana na taarifa hiyo ya uchambuzi wa takwimu, imeeleza kuwa idadi iliyotumika kutoa maoni ya watanzania ni 351,664 idadi ambayo haiwezi kuwakilisha watanzania wengine milioni 45, ikiwa pamoja na tafasiri shinikizo ya takwimu (muungano badala ya mambo mengine), huku sababu ya kutokea mapungufu hayo katika ukusanyaji maoni hayo ikielezwa kaitka taarifa hiyo ya uchambuzi wa Bituro, kuwa ni muda mdogo, bajeti  finyu, tume kutaka kutokinzana na wanaharaki pamoja na tume kuendeshwa na mhaniko wa hisia za wajumbe wake.
 Mchambuzi na mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii Paschal Bituro Kazeri

Wakati ikiundwa tume hiyo ya kuandaa rasimu mpya ya katiba , watanzania waliaminishwa kuwa wakati ulikuwa umefika wa kuandika katiba upya kwa kile kile kilichoelezwa kuwa katiba ya sasa iliandikwa na watu wachache kutokana wananchi kutoshirikishwa, ilimpa rais madaraka makubwa ikiwa ni pamoja na kuonesha kuwa tume ya uchaguzi sio huru na haki na kwasababu hiyo chaguzi zote zinazosimamiwa na tume ya uchaguzi hazitoi mshindi anayekuwa amchaguliwa na wananchi, hivyo utayarishaji wa katiba mpya ulipaswa kurekebisha mapungufu hayo, kitu ambacho imeshindwa na kurudia yaleyale.

Kutolewa kwa taarifa hiyo ya uchambuzi ya takwimu za ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni kutaka kuionesha nia nzuri tume kuwa walifikia vipi katika kutoa rasimu mpya ya katiba tarajiwa, na kuongeza kuwa taarifa hiyo inajnga msingi mzuri wa kuikosoa tume ya warioba na hivyo kufuta mawazo miongoni mwa watanzania kuwa hoja zao ziliwekwa kapuni.

Saturday 1 March 2014

MASHINDANO YA SOKA LA VIJANA TANZANIA YAANZA MWANZA, JUMLA YA TIMU 12 KUTOKA MIKOA YA TANZANIA BARA YASHIRIKI KATIKA MASHINDANO HAYO.


Mashindano ya soka ya vijana nchini Tanzania yaanza Mwanza hapo jana huku yakishirikisha ujmla ya mikoa 12 ya Tanzania bara. 

 Mashindano hayo yameandaliwa na Alliane school academy ya Mwanza huku yakifunguliwa na Ayoub Nyenzi, mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana kutoka shilikisho la soka nchini Tanzania TFF.

Katika mchezo wa ufunguzi wenyeji Alliance walianza vyema baada ya kuwafunga timu ya Future kutoka Arusha mabao 2 - 1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.

Akifungua mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka, mwenyekiti wa kamati ya soka loa vijana kutoka TFF, Ayoub Nyenzi amesema kuwa litayaweka katika kalenda yake mashindano hayo ili kuyaongezea hamasa mashindano hayo, yenye lengo la kuibua vipaji vya soka kwa vijana nchini Tanzania.

Nyenzi aliwataka vijana kuondokana na tabia ya utumiaji mihadarati kama kweli wanataka kuliendeleza soka lao.

Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana kutoka TFF, Ayoub Nyenzi wakati akifungua mashindano ya soka la vijana kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 Timu shiriki zikishiriki katika mandamano ya mashindano hayo yaliyoanzia kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana kuelekea CCM Kirumba, ijumaa iliyopita.