Sunday 2 March 2014

RIPOTI YA JAJI WARIOBA KUHUSU RASIMU MPYA YA KATIBA YAENDELEA KUPONDWA >>>>>>>

   Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Rasimu ya Katiba Mpya Jaji Joseph Sinde Warioba



Licha ya tume ya mabadiliko ya rasimu mpya ya katiba nchini Tanzania kukamilisha kazi yake,
bado yaendelea kukosolewa -Bituro
·    Yaelezwa maoni yaliyokusanywa yanamapungufu makubwa.
·    Idadi ya waliotoa maoni hakidhi na haiwezi kuwakilisha watanzania milioni 45.

Na. Deo Kaji Makomba.

Wakati  wajumbe wa bunge maalum la katiba wakiendelea na mkutano wa utungaji kanuni alkadharika majadiliano kuhusu rasimu ya katiba mpya iliyoandaliwa na tume maalum ya katiba iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake jaji Joseph Sinde Warioba, wananchi  mbalimbali wamezidi kuikosoa rasimu ya katiba.

Kwa mujibu wa taarifa ya uchambuzi wa takwimu za maoni ya wananchi ya rasimu ya katiba mpya uliofanywa  na Paschal Bitulo Kazeri  ambaye ni mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii na nakala yake kukifikia Kisima chetu  cha habari, imeeleza kuwa,  nia ama malengo ya kufanya mabadiliko ya katiba mpya ni mazuri kwani katiba iliyopo ama kwa hakika imepitwa na wakati na hivyo kutokwendana na wakati wa sasa.

Katika taarifa yake hiyo ya uchambuzi, Bituro ameleza kuwa licha ya tume ya jaji wariomba kumaliza kazi yake, imeonesha mapungufu makubwa na kwamba haiakisi maoni na na takwimu za maoni ya watanzania.
Kulingana na taarifa hiyo ya uchambuzi wa takwimu, imeeleza kuwa idadi iliyotumika kutoa maoni ya watanzania ni 351,664 idadi ambayo haiwezi kuwakilisha watanzania wengine milioni 45, ikiwa pamoja na tafasiri shinikizo ya takwimu (muungano badala ya mambo mengine), huku sababu ya kutokea mapungufu hayo katika ukusanyaji maoni hayo ikielezwa kaitka taarifa hiyo ya uchambuzi wa Bituro, kuwa ni muda mdogo, bajeti  finyu, tume kutaka kutokinzana na wanaharaki pamoja na tume kuendeshwa na mhaniko wa hisia za wajumbe wake.
 Mchambuzi na mtafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii Paschal Bituro Kazeri

Wakati ikiundwa tume hiyo ya kuandaa rasimu mpya ya katiba , watanzania waliaminishwa kuwa wakati ulikuwa umefika wa kuandika katiba upya kwa kile kile kilichoelezwa kuwa katiba ya sasa iliandikwa na watu wachache kutokana wananchi kutoshirikishwa, ilimpa rais madaraka makubwa ikiwa ni pamoja na kuonesha kuwa tume ya uchaguzi sio huru na haki na kwasababu hiyo chaguzi zote zinazosimamiwa na tume ya uchaguzi hazitoi mshindi anayekuwa amchaguliwa na wananchi, hivyo utayarishaji wa katiba mpya ulipaswa kurekebisha mapungufu hayo, kitu ambacho imeshindwa na kurudia yaleyale.

Kutolewa kwa taarifa hiyo ya uchambuzi ya takwimu za ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni kutaka kuionesha nia nzuri tume kuwa walifikia vipi katika kutoa rasimu mpya ya katiba tarajiwa, na kuongeza kuwa taarifa hiyo inajnga msingi mzuri wa kuikosoa tume ya warioba na hivyo kufuta mawazo miongoni mwa watanzania kuwa hoja zao ziliwekwa kapuni.

Saturday 1 March 2014

MASHINDANO YA SOKA LA VIJANA TANZANIA YAANZA MWANZA, JUMLA YA TIMU 12 KUTOKA MIKOA YA TANZANIA BARA YASHIRIKI KATIKA MASHINDANO HAYO.


Mashindano ya soka ya vijana nchini Tanzania yaanza Mwanza hapo jana huku yakishirikisha ujmla ya mikoa 12 ya Tanzania bara. 

 Mashindano hayo yameandaliwa na Alliane school academy ya Mwanza huku yakifunguliwa na Ayoub Nyenzi, mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana kutoka shilikisho la soka nchini Tanzania TFF.

Katika mchezo wa ufunguzi wenyeji Alliance walianza vyema baada ya kuwafunga timu ya Future kutoka Arusha mabao 2 - 1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.

Akifungua mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka, mwenyekiti wa kamati ya soka loa vijana kutoka TFF, Ayoub Nyenzi amesema kuwa litayaweka katika kalenda yake mashindano hayo ili kuyaongezea hamasa mashindano hayo, yenye lengo la kuibua vipaji vya soka kwa vijana nchini Tanzania.

Nyenzi aliwataka vijana kuondokana na tabia ya utumiaji mihadarati kama kweli wanataka kuliendeleza soka lao.

Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana kutoka TFF, Ayoub Nyenzi wakati akifungua mashindano ya soka la vijana kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 Timu shiriki zikishiriki katika mandamano ya mashindano hayo yaliyoanzia kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana kuelekea CCM Kirumba, ijumaa iliyopita.







Friday 7 February 2014

AFRIKA NA SAFARI YA KUELEKEA NCHINI BRAZIL.



Afrika na safari ya kuelekea nchini Brazil.
·    Ni katika kinyang’anyiro cha kuwania kombe  la dunia.
·    Macho na masikio ya wapenzi wa soka duniani kuelekezwa Brazil mwaka huu.

Na. Josephat Kaira.




Kamakawaida wewe shabiki mkubwa wa kisima cha burudani tunaendelea kufahamishana habari kemkem za kiburudani  zinazoendelea katika ulimwengu wa burudani  kama tulivyoanza  awali kukufahamisha  kukamilika kwa baadhi ya viwanja vitakavyotumika katika kipute kijacho cha kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2014 nchini Brazil sasa tunakufahamisha vikosi vya timu shiriki na nyota wake na leo hii tunaanzia na wawakilishi toka barani afrika ambapo bara hilo linawakilishwa na timu tano.

Cameroon   simba wasioshindika  simba wanyika  ni miongoni  mwa timu zitakazo iwakilisha Africa katika michuano hiyo huko brazil ikiongozwa na kocha Volker  Finke na itakuwa ikimtegemea zaidi nyota wake Samwel etoo Phil anayekipiga kwenye club ya Chelsea ya England kama chachu ya ushindi pamoja na wachezaji wengine kama akina Steven mbia anayecheza soka la kulipwa kwenye club ya Olympic maseyii ya nchini ufaransa,joel matip anayekipiga na shalke 04 ya ujerumani na wengineo wengi.

Timu ya Taifa ya Cameroon

Ghana maarufu kama black stars brazil ya Africa mashabiki wa soka barani Africa waliweza kuthubutu kuiita hivyo kutokana  na soka ya kutandaza pasi za uhakika itaongozwa na kocha James Kwesi Appiah na watakuwa  na vifaa wao akina Michael essien Asamoa Gyan Sule muntari na wengineo wao watakuwa kundi  G na timu za  ujerumani,ureno pamoja na marekani.

 Timu ya Taifa ya Ghana

Ivory coasty hawa ni tembo maarufu wakifahamika hivyo ni timu nyingine itakayo iwakilisha Africa katika michuano hiyo ya kombe la dunia kwa mwaka 2014 nchini brazil itakuwa ikinolewa na  Sabri lomauchi na ikiwategemea nyota wake kama Didier drogba Yaya toure nduguye kolo toure itakuwa kundi c pamoja na timu za  Colombia,Ugiriki na japani.

Timu ya Taifa ya Ivory Coast

Algeria maarufu kama mabwea wa jangwani  fennec   foxes  hawa ni wawakilishi wengine kutoka kaskazini mwa bara la Africa wakiwa na kocha wao Vahid  Halihodzic na watakuwa wakiwategmea akina  majid boughera anayekipiga kweny club ya  lekhwiya,ryad  boudebouz anayekipiga katika timu ya bastia ya nchini ufaransa ambapo watakuwa na upinzani mkali na timu za  urusi ubelgiji na jamhuri ya watu wa korea katika kundi h.

 Timu ya Taifa Algeria

Nigeria super eagles wakiwa na kocha mzalendo na aliyepata mafaniko makubwa na timu hiyo kwa siku za karibuni baada ya kunyakuwa ubingwa wa Africa Steven keshi wao watakuwa na matumaini makubwa kwani wanajivunia kikosi kilichosheheni nyota kibao wanaosakata kandanda la kulipwa barani ulaya kama akina John mikel Obi,Uche, mlinda mlango Vicent Enyeama na wengineo  ambao watakuwa nchachu ya ushindi katika mechi zao za kundi  f wakiwa na timu za Argentina,Boznia and Herzegovina na iran.

 
Timu ya Taifa ya Nigeria

Thursday 6 February 2014

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA NCHINI BRAZIL 2014 MAANDALIZI YA VIWANJA YAENDELEA KUKAMILIKA

Na. Josephat Kaira.


Kama kawaida yetu kisima cha burudani kinaendelea kukupatia mambo mazuri kuhusiana na burudani kitaifa na kimataifa ,zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuanza kivumbi  cha soka cha kombe la dunia kwa mwaka 2014 nchini brazil kitakacho shirikisha timu 32 tumeona ni vizuri tukaanza kukufahamisha viwanja ambavyo vitakuwa vikitumika katika michuano hiyo mikubwa.
Arena de sao  Paulo

Uwanja wa kwanza ni  arena de sao  Paulo,huu ni uwanja ambao uko mjini kabisa katika jiji la sao Paulo hili ni jiji maarufu na lenye idadi kubwa ya watu na linategemewa kubeba idadi kubwa ya mashabiki kutoka kona mbalimbali za dunia  unachukua idadi ya watu  65,807 unamaliziwa vizuri mwezi huu wa februari na cha kukuongezea ni kuwa wakati wa matengnezo yake hivi karibuni uliua wajenzi wawili katika ajali iliyotokea wakati wa ujenzi wa uwanja huo novemba 27 mwaka jana.

Uwanja mwingine utakaotumika katika kipute hicho ha kombe la dunia mwaka 2014 nchini brazil ni estadio mineirao bero herizonte huu ni miongoni mwa viwanjab vikongwe vya soka nchini brazil ulijengwa mwaka 1965 lakini ukafanyiwa ukarabati mkubwa mwaka 2013 lengo likiwa ni kuuweka sawa kabla ya michuano hiyo  kuanza,unachukua mashabiki  62,547 uko miles kutoka rio de geneiro.
 Estadio mineirao bero herizonte

Tukiwa tunendelea kuahamishana viwanja vingine ambavyo vitkuwa vikitumika katika michuano ya kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2014 baada ya hivyo viwili vya hapo juu estadio costelao Fortaleza huu ulianza kutumika mwaka 1973 ukafanyiwa ukarabati mkubwa mwaka 2013 unabeba mashabiki wapatao 64,846.
 Estadio costelao Fortaleza

Uwanja  mwingine ni estadio maracana rio de janairo huu ni uwanja mwingine baab kubwa ambao nchi ya brazil itakuwa ikijisifia katika michuano hiyo huko jijini rio de janairo kwa watoto wa mujini vilevile unavikolombezo vingi pia unabeba mashabiki wengi wapatao 76,804 kuzidi ata viwanja vingine tulivyotangulia kukuelezea apo awali.
 Estadio-maracana

Estadio nacional brasilia  huu unachukua mashabiki 68,009 ulifunguliwa mwaka 1974 ila ukaanyiwa tena ukarabati mwaka 2013 mwezi may.
 Estadio-Nacional-de-Brasilia-Julio-Cecilio

Kwa leo tutahitimisha na kukufamisha uwanja wa  arena pernambuco recife huu ni uwanja mpya kabisa ukijengwa hivi karibuni na kufunguliwa mwaka 2013 mwezi may na unachukua mashabiki wapatao 44,248 ni moja kati ya viwanja vitakavyo nogesha michuano hiyo kwani kwa nje kina muwako muwako furani wa kupendeza.


Arena pernambuco recife usiku

Naam kwa wewe unae endelea  kutufuatilia wana kisima cha burudani tutakutajia viwanja vingine vitakavyotumika katika kipute cha kombe la dunia mwaka huu nchini  brazil kadri tuwezavyo endelea kuwa nasi.

Naye mshambuliaji dimitar berbatov amebainisha kuwa mlinzi wa Manchester united mfaransa Patrice evra ndiye aliyemshawishi kujiunga na club ya Monaco katika kipindi cha usajili cha mwezi uliopita wa januari.

  Berbatov

Berbatov raia wa burigaria amesema kuwa rafiki yake evra waliyekuwa wakicheza wote Manchester united kati ya mwaka 2008 hadi 2012 ndiye aliyemwambia mambo mazuri yaliyopo Monaco na kumshawishi kujiunga nayo kwa mkopo akiziba pengo la mkolombia radamel falcao aliye majeruhi.